CHAKIKA WAHUDHURIA KONGAMANO LA CHAWAKAMA (KENYA) KATIKA CHUO KIKUU CHA K.A.G – EAST KIJIADO

Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Karatina CHAKIKA walihudhuria Kongamano lililofana la CHAWAKAMA – Kenya, (Chama cha Wanafunzi wa Kiswahili, Vyuo Vikuu Afrika Mashariki – Kenya) lililofanyika tarehe 6 na 7 Machi 2026 katika Chuo Kikuu cha K.A.G East Kajiado.  Kongamano hili hupangwa kila mwaka na hushikrikisha wanafunzi  wa Kiswahili wa Vyuo Vikuu vya Afrika Mashariki. Kaulimbiu ya kongamano hilo ilikuwa: Nafasi ya Kiswahili katika Mtaala wa Elimu ya Kiumilisi (C.B.E). Idadi ya wanafunzi waliohudhuria kutoka vyuo mbalimbali walikuwa 3000. Makongamano kama haya ni muhimu kwa wanafunzi kwa sababu hukuza vipawa wanafunzi, kubadilishana fikra na mawazo na pia kuchangiana kuhusu taaluma zao.

Ni hadhi kubwa kwa Chuo Kikuu cha Karatina kuwakilishwa na wanafunzi 61. Katika kongamano hili wanfunzi waliandamana na Prof. Joseph N. Maitaria ambaye ni Mlezi wao. Wanafunzi walipata fursa ya kuwasilisha makala yao yenye mada: Nafasi ya Mitandao ya Kijamii katika Kuendeleza Kiswahili katika Mtaala wa Elimu ya Kiumilisi. Prof. Maitaria alitunukiwa nafasi muhimu ya kuwahutubia wanafunzi ambao alitilia mkazo wanafunzi kujitahidi katika masomo yao ya Shahada ya Kwanza ili wapate fursa ya kujiunga na masomo ya uzamili katika Chuo Kikuu cha Karatina. Katika Kongamano hilo ilipendekezwa kuwa kongamano lijalo la Novemba 2026 litafanyika katika Chuo Kikuu cha Karatina. Heshima kubwa hii kwa Chuo Chetu teule cha Karatina. Sote tunawahongera wanafunzi wetu katika kutuwakilisha katika ngazi ya kitaifa na kimataifa.

 

Kwa sasa Chama cha Kiswahili cha Karatina (CHAKIKA) kinaongozwa na wanafunzi wafuatao:

Bi. Caren Keter, Bi. Bridgid Chepkirui,Bi. Purity Njeri, Bw. Dennis Ngatia, Bw. Kenneth Koech, Bw. Michael Omari, Bw. Amos Kiptoo, Bw. Benjamin Otaigo na Bw. Amon Kipng’etich.

 

Prof. Joseph N. Maitaria

Mlezi wa Chakika